MABADILIKO YA TAREHE YA KUFUNGUA CHUO

MKUU WA CHUO, CHUO CHA MAFUNZO YA UFUGAJI NYUKI – TABORA ANAWATANGAZIA WANACHUO WOTE WANAOENDELEA NA MASOMO KWA MWAKA WA MASOMO WA 2021/2022 KUWA TAREHE YA KUFUNGUA CHUO IMEBADILIKA KUWA TAREHE 01 NOVEMBA 2021 NA SIO TAREHE ILIYOPO KATIKA KALENDA YA CHUO YA MWAKA 2020/2021.

HIVYO WANAFUNZI WOTE WANATAKIWA KURIPOTI CHUONI TAREHE 01 NOVEMBA 2021 ILI KUENDELEA NA MASOMO KWA MWAKA WA MASOMO WA 2021/2022. AIDHA UONGOZI WA CHUO UNAOMBA RADHI KWA USUMBUFU WOWOTE UTAKAOSABABISHWA NA MABADILIKO HAYA.