TANGAZO LA MASOMO YA MUDA MFUPI(SHORT COURSE) SEPTEMBA 2025

Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki Tabora kinapenda kuwajulisha kuwa
Kutakuwa na Mafunzo ya ufugaji Nyuki ya muda mfupi (Short course) yatakayo
endeshwa chuoni kuanzia mwezi Septemba, 2025. Kozi hii imelenga kutoa
elimu ya kitaalamu kwa watu binafsi, vikundi vya vijana, wanawake, wakulima,
na wajasiriamali wanaopenda kuanza au kuboresha shughuli za ufugaji wa
nyuki kwa ajili ya kuongeza kipato na kulinda mazingira. Muda wa mafunzo ni siku tano (5), kuanzia tarehe 8 hadi 12 Septemba 2025. Pakua fomu hapa