MABADILIKO YA TAREHE YA KUANZA MITIHANI YA MARUDIO

Mkuu wa Chuo anapenda kuwatangazia wanachuo wote kuwa; mitihani ya marudio (supplementary examinations) ya muhula wa II mwaka wa masomo 2022/2023 itafanyika kuanzia Jumatatu tarehe 18 Septemba 2023 badala ya tarehe 25 Septemba 2023 kama ilivyokuwa imepangwa awali.

Mabadiliko haya yanatokana na sababu mbalimbali ikiwemo kubadilika kwa taratibu za utoaji matokeo. Hivyo basi Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

USOMAPO TANGAZO HILI, MJULISHE NA MWINGINE