Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki Tabora kinapenda kuwajulisha kuwa
Kutakuwa na Mafunzo ya ufugaji Nyuki ya muda mfupi (Short course) yatakayo endeshwa chuoni mwezi Septemba, 2025. Kozi hii imelenga kutoa elimu ya kitaalamu kwa watu binafsi, vikundi vya vijana, wanawake, wakulima,na wajasiriamali wanaopenda kuanza au kuboresha shughuli za ufugaji wa
nyuki kwa ajili ya kuongeza kipato na kulinda mazingira. Muda wa mafunzo ni siku tano (5), kuanzia tarehe 8 hadi 12 Septemba 2025. Pakua fomu hapa
Author Archives: nyuki-tabora
WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA NA TAMISEMI KUJIUNGA NA CHUO KWA MWAKA WA MASOMO 2025/2026
Mkuu wa Chuo anawapongeza na kuwakaribisha wanafunzi wote waliochaguliwa na tamisemi kujiunga na chuo cha mafunzo ya ufugaji nyuki Tabora(BTI). Kuona majina ya wanafunzi waliochaguliwa na TAMISEMI bofya hapa
TANGAZO LA NAFASI ZA MASOMO 2025/2026
Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki-Tabora anatangaza nafasi za
masomo katika fani ya Ufugaji Nyuki kwa ngazi ya Astashahada na
Stashahada kwa mwaka wa masomo 2025/2026. Kwa vigezo na masharti bofya hapa. Kupakua fomu ya maombi bofya hapa.